AFCONAfricaAfrika MasharikiNyumbani
Msigwa akabidhi mil10 za goli la Mama

MSEMAJI mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ametimiza ahadi ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kununua kila goli litakalofungwa na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwenye michezo yake ya kampeni ya kuisaka nafasi ya kucheza michuano ya mataifa ya Afrika ‘Afcon’
Rais Samia aliahidi kulinunua kila goli kwa shilingi milioni 10 na leo msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa amemkabidhi fedha hizo mfungaji wa goli la siku ya jana kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger Simon Msuva.
Taifa Stars tayari imetanguliza mguu mmoja kwenye michuano hiyo kwani inahitaji alama moja tuu ili kufuzu kwenye michuano hiyo itakayofanyika mwakani nchini Ivory coast.