Ligi Daraja La Kwanza

Msheri: Kombe la Muungano tunalitaka

PEMBA: BAADA ya kufanikiwa kufuzu kwa hatua ya fainali ya Kombe la Muungano, kipa wa Yanga, Abdultwali Msheri, amesema wamefanya maandalizi ya hali ya juu kuelekea mchezo wao dhidi ya JKU kutoka Zanzibar.

Fainali hiyo inayotarajiwa kupigwa kesho katika Uwanja wa Ngombani, Pemba, inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka kutoka pande zote mbili za Muungano.

Yanga ilikata tiketi ya fainali baada ya kuwatoa Zimamoto kwa mikwaju ya penalti kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 za mchezo huo.Kwa upande wao, JKU waliwatoa Azam FC na kujiweka katika nafasi nzuri ya kugombea taji hilo.

Akizungumza baada ya mechi ya nusu fainali, Msheri alikiri kuwa mchezo dhidi ya Zimamoto ulikuwa mgumu lakini uliwajenga na kuwaweka tayari kwa changamoto kubwa zaidi.

“Tumejifunza mengi kupitia mechi hiyo. Sasa akili zetu zote zimeelekezwa kwa fainali. Tumejipanga kuhakikisha kombe linavuka maji na kurejea Dar es Salaam,” amesema

Msheri pia aliwataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao, akiahidi kuwa watafanya kila wawezalo kuwapa furaha na kuwahakikishia ushindi.

Related Articles

Back to top button