Tetesi

Mourinho amtaka Son Heung-Min

ISTANBUL:JOSE Mourinho, kocha wa Fenerbahce, anapanga kumsajili nyota wa Tottenham Hotspur, Son Heung-min, kwa mujibu wa ripoti mbalimbali

Mourinho, ambaye amekuwa akitumia uzoefu wake wa Ligi Kuu ya Uingereza kuimarisha kikosi cha Fenerbahce kwa kusajili wachezaji kama Allan Saint-Maximin na Caglar Soyuncu, sasa anataka kuongeza nguvu zaidi ili kufikia kiwango cha wapinzani wao Galatasaray.

Son, nahodha wa Tottenham, anasemekana kuwa kwenye orodha ya kwanza ya Mourinho kwa usajili wa dirisha la Januari. Mkataba wa Son na Spurs unamalizika Juni, na bado hakuna mazungumzo ya kusaini mkataba mpya, hali inayowapa Fenerbahce nafasi ya kumnasa kwa dau dogo au hata bure mwishoni mwa msimu.

Pia, Mourinho anavutiwa na mshambuliaji wa Chelsea, Joao Felix, pamoja na kiungo Nicola Zalewski wa Roma, ambaye anaweza kuwa mchezaji rahisi zaidi kusajili kwa dau la € milioni 5. Hata hivyo, Mourinho anakabiliwa na ushindani kutoka klabu kubwa kama Barcelona na Bayern Munich ambao pia wanammezea mate Son.

Related Articles

Back to top button