Tetesi

Šeško aziacha solemba Arsenal, Chelsea, Man Utd

Benjamin Sesko anatarajia kuongeza mkataba na kusalia klabuni RB Leipzig,Sky Sports na Fabrizio Romano wanaripoti.

Straika huyo kutoka Slovenia amekuwa akihusishwa na vilabu vikubwa kama vile Arsenal,Chelsea,Tottenham na Manchester United.

Hata hivyo, Sesko atasaini kandarsai mpya iliyoboreshwa zaidi na timu hiyo kuelekea michuano ya Euro 2024.Timu yake ya Taifa ya Slovenia itamenyana na England,Denmark na Serbia katika hatua ya makundi.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 21 tu,aliifungia Leipzig jumla ya mabao 18 katika michuano yote huku magoli 7 akiyafunga katika michezo 7 ya mwisho ya Bundesliga.

Related Articles

Back to top button