Tetesi

Tetesi za usajili

KLABU ya Chelsea iko tayari kumruhusu Mykhailo Mudryk kuondoka kwa mkopo timu hiyo wakati wa dirisha la uhamisho Januari, 2024 baada ya kushindwa kuonesha ubora wake Stamford Bridge.(Fichajes)

Real Madrid inataka kumuunganisha Jude Bellingham na mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Youssoufa Moukoko iwapo itashindwa kumsajili Kylian Mbappe kutoka Paris Saint-Germain.(Defensa Central via Football Transfers)

Golikipa David de Gea huenda akastaafu soka iwapo atashindwa kupata ofa kuwa mlinda lango namba moja kwenye klabu kubwa barani Ulaya. (The Guardian)

Wachezaji kadhaa wa Manchester United hawakubaliani na uamuzi wa kocha Erik ten Hag kumfukuza Jadon Sancho kwenye kikosi cha kwanza.(talkSPORT)

Barcelona huenda ikaingia kwenye kinyang’anyiro na Tottenham kuwania saini ya mshambuliaji wa Nigeria, Gift Orban ambaye anafunga mabao kwa kiwango kikubwa akiwa na Gent katika Ligi ya Kuu ya Ubelgiji.(Fichajes)

Related Articles

Back to top button