Habari Mpya

Morocco aiwazia Nigeria

BAADA ya timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 ‘Ngorongoro Heroes’ kusonga mbele hatua ya pili kufuzu Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika-AFCON) Kocha Mkuu Hemed Morocco amesema kitu cha msingi sasa ni kupata maandalizi ya kutosha ambayo anaamini ndiyo silaha kubwa ya kuivusha timu kwenda raundi ya tatu.

Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Hemed Morocco.

 

Akizungumza na Spotileo Morocco amesema mchezo dhidi ya Sudan Kusini ulikuwa mgumu lakini kilichosaidia ni Ngorongoro Heroes kucheza kwa kufuata maelekezo aliyowapa.

“Nawapongeza sana wachezaji wangu sababu walicheza kwa kujitoa kutafuta ushindi hasa ukizingatia Sudan Kusini walikuwa hawana cha kupoteza ukweli nafurahi kuona tumesonga mbele,” amesema Morocco.

Amesema anatambua mchezo unaofuata dhidi ya Nigeria utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzania wao.

Katika mchezo huo uliopigwa Rwanda Ngorongoro ilitoka sare ya mabao 3-3 na kusonga mbele kwa faida ya bao la ugenini kufuatia mchezo wa kwanza uliochezwa Tanzania timu hizo kutoka suluhu.

Related Articles

Back to top button