
MWANAMUZIKI Awadhi Chami maarufu Moni Centrozone amesema tangu aanze kuwa
kwenye mahusiano ya kimapenzi hajawahi kufi kiria kumvisha pete yeyote kati ya wote
aliowahi kuwa nao kutokana na sababu mbalimbali.
Moni ameliambia gazeti la HabariLEO kuwa hilo linatokana na sababu nyingi ikiwemo suala
la dini, mazingira yake binafsi, mazingira ya aliyenaye na vitu vingine.
“Niwe muwazi, sijawahi kuwaza kumvisha mtu pete kwa sababu wasichana wengi niliokuwa
nao walikuwa dini tofauti na mimi kwa hiyo sikuwahi kulifikiria hilo, kuna muda naangalia
mazingira yangu na yake nasema hapana hapa sidhani kama panafaa,” amesema Moni.
Moni mwenyeji wa Dodoma ameeleza kuwa kwa sasa yuko kwenye uhusiano mpya, hivyo
anatazama mwenendo na vitu vingi akimpa muda mpenziwe huyo kabla ya kufikiria suala la kumvisha hata pete ya uchumba.
“Sasa hivi nipo na mahusiano mapya naangalia kipi kitanishawishi kwa mtu wangu, lazima umpe nafasi na muda kidogo kwa ajili ya kuhakikisha unachokifanya kinaendana na
mapenzi mliyonayo,” amesema Moni.