Mastaa
Mobetto amwagia sifa Aziz Ki

DAR ES SALAAM: MWANAMITINDO, Hamisa Mobetto, amemwagia sifa mume wake Stephane Aziz Ki, alipokuwa akimtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mobetto ameandika ujumbe mrefu wa upendo na shukrani akimpongeza mumewe kwa umri mpya, huku akieleza namna anavyothamini uwepo wake katika maisha yake.
“Nakupenda sana mume wangu halali wa ndoa takatifu. Kila siku namshukuru Mungu kwa ajili yako na kwa baraka ya kuwa na wewe maishani mwangu,” aliandika Mobetto
Ujumbe huo wa kimahaba umevutia hisia za mashabiki wengi mitandaoni, waliomiminika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwapongeza na kuwatakia heri wanandoa hao.




