Ligi Kuu

Kitendawili nafasi ya 2, mfungaji bora kuteguliwa leo

KITENDAWILI cha timu itayoungana na Yanga katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kitateguliwa leo wakati ligi inafikia tamati.

Azam na Simba zote zina pointi 66, lakini zinatofautiana mabao ya kufunga na kufungwa Azam ikikusanya mabao 61 wakati Simba ina 57.

Timu yoyote kati ya hizo itakayofungwa au kutoka sare itacheza Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Lakini zikitoka sare Azam itanufaika na idadi kubwa ya mabao  na iwapo Simba haitashinda zaidi ya 6.

Katika vita ya mfungaji bora, Stephanie Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum wa Azam wote wana mabao 18 na ni michezo ya mwisho leo itakayoamua mchezji yupi atachukua kiatu cha dhahabu.

Vita ya kuepuka kushuka daraja imebaki kwa timu mbili, Tabora United yenye pointi 27 na Geita Gold yenye 25 wakati Kagera Sugar yenye pointi 31 italazimiaka kushinda mchezo ili kuepuka kucheza mtoani kubaki Ligi Kuu.

Michezo ya kumaliza ligi hiyo leo ni kamqa ifuatavyo:

Yanga vs Tanzania Prisons
Simba vs JKT Tanzania
Geita Gold vs Azam
Coastal Union vs KMC
Ihefu vs Mtibwa Sugar
Mashujaa vs Dodoma Jiji
Namungo vs Tabora United
Singida Big Stars vs Kagera Sugar

Related Articles

Back to top button