Mkali wa Dancehall, Shaggy na baraka za Mungu

JAMAICA: MKALI wa wimbo wa ‘It Wasn’t Me’, Orville Burrell maarufu Shaggy amesisitiza kuwa yeye hahusiki na kuandika wimbo wake wowote bali anaamini nyimbo zote za kuvutia alizotoa zimetokana na Mungu wake zikiwa kama njia ya kusaidia watu wengine.
Shaggy ameliambia gazeti la Daily Star Sunday: “Watu wanasema niliandika ‘It Wasn’t Me’ na vibao vyangu vingine lakini sikuandika hata kimoja.
“Kama ingetoka kwangu basi ningeandika kibao kimoja kila wiki. Ninaamini kwa dhati nyimbo hizo zilitolewa kwangu kusaidia kubadilisha maisha ya watu. Niko hapa kufanya huduma hadi sihitajiki tena.”
Shaggy ambaye jina lake halisi ni Orville Burrell anajivunia kuwa katika muziki kwa zaidi ya miaka 30 baada ya kupata mafanikio ya haraka baada ya wimbo wake wa kwanza na ‘Oh Carolina’ wa mwaka 1993.
Amesema: “Imekuwa ni safari ya kutosha. “Hakuna wasanii wengi ambao wanapata mafanikio zaidi ya miongo mitatu ya muziki. “Nakumbuka baada ya ‘Oh Carolina’ waliniita ‘the one hit wonder’.
“Kisha nilifanya ‘Boombastic’ na mimi ndiye niliyefanya wimbo mwingine mkali kisha nikatoa ‘Summertime’. “Wakati huo hakuna mtu ambaye alikuwa ameona msanii wa dancehall akiwa na nyimbo zinazofuata na kali.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 56 hapo awali alitajwa kupumzika kufanya muziki kutokana na mambo mengine, kama vile kuendesha kipindi cha ‘The Little Mermaid Live’ mwaka 2019.