Mapinduzi CupNyumbani
Michuano ya Mapinduzi yapamba moto
MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Zanzibar imepambana moto huku leo zikipigwa mechi mbili.
Mchezo wa awali Jamhuri itaivaa Azam na kisha baadaye Simba ambayo inakamilisha ratiba baada ya kuvuliwa ubingwa ikikiwasha na KVZ.
Michezo hiyo inafanyika uwanja wa Amaan mjini Unguja.
Katika michezo miwili iliyopigwa Januari 4 Yanga imeichapa KMKM kwa bao 1-0 wakati Namungo na Chipukizi zimetoka suluhu.




