Michael B Jordan Kupokea Tuzo ya 39 ya Sinema za Amerika

NEW YORK: MUIGIZAJI wa ‘Sinners’ Michael B. Jordan pamoja na juhudi zake za uhisani kupitia Ushirika wake wa Lutlier Society Fellowship na mashindano ya mpira wa Kikapu ya HBCU Legacy Classic, anatarajiwa kutunukiwa Tuzo ya 39 ya Sinema ya Marekani.
Tuzo hiyo inatarajiwa kutolewa katika sherehe maalum katika Hoteli ya Beverly Hilton huko California mnamo Novemba 20.
Mwenyekiti wa bodi ya Cinematheque ya Marekani, Rick Nicita amesema katika taarifa yake kwamba: “Kazi ya Michael B. Jordan imekuwa onesho lisilo na kifani kwa mchanganyiko wa talanta bora na maono yenye kusudi ambayo yamemfanya kuwa na nguvu kubwa katika biashara ya sinema ya leo.
“Aliingia katika filamu na ‘Fruitvale Station’ kasha akaifuata ‘Black Panther’ na filamu tatu za ‘Creed’, pia akafanya utayarishaji wake wa kwanza katika ‘Creed III’, huku akiendelea na juhudi zaidi za kuwa muongozaji bora wa filamu.
“Amekuwa mtayarishaji mzuri na miradi mingi katika biashara yetu na shughuli zake za uhisani ni nyingi kama hivi karibuni katika ‘Sinners’ imeimarisha mno mfumo wake wa uandaaji wa filamu na kuonyesha taswira njema kwa wakati ujao.
“The American Cinematheque inajivunia kuwasilisha Tuzo ya 39 ya Sinema ya Kimarekani kwa Michael B. Jordan.”
Hafla hiyo ni uchangishaji wa kila mwaka kwa shirika lisilo la kiserikali la Cinematheque la Amerika na mwaka jana lilimtukuza tuzo ya 38, Jessica Chastain.
Wasanii wengine waliowahi kutunukiwa tuzo hiyo ni pamoja na Robert Downey Jr., George Clooney, Al Pacino, Charlize Theron, Nicole Kidman, Denzel Washington, Ryan Reynolds na Dame Helen Mirren.
Nyota wa Hollywood, Tom Cruise, alisifu kazi ya Michael, haswa ushirikiano wake na Ryan Coogler, mapema wiki hii.
Akiongea na ‘Extra’, Tom anaamini Michael, 38, ni mwigizaji mwenye talanta kubwa, na angependa kufanya kazi naye siku moja.