Ligi KuuNyumbani

Mgunda asikitika Simba kupata sare

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda.

KAIMU Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema kukosa ushindi katika mchezo dhidi ya Singida Big Stars, Novemba 9 kumepunguza matumaini ya kuzoa pointi zote 18 katika mechi sita mwezi huu.

Akizungumza na SpotiLeo baada ya timu hiyo kuwasili mkoani Dodoma kocha huyo amesema kutokana na malengo ushindi ulikuwa ni muhimu lakini Simba imejikuta ikipata pointi moja kutokana upinzani wa Singida Big Stars.

“Imetuumiza kupata sare sababu siyo malengo yetu, tunajipanga kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mechi zijazo ambazo naamini tutashinda,” amesema Mgunda.

Mgunda amewataka wachezaji kuendelea kupambana na mashabiki kuipa sapoti timu hiyo ili kufanya vizuri kwenye mashindano yote inayoshiriki msimu huu.

Simba kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 18 baada ya michezo 9.

Related Articles

Back to top button