Habari Mpya

Mechi zimeimarisha kikosi-Rweyemamu

MENEJA wa klabu ya Simba, Patrick Rweyemamu amesema mechi mbili ilizocheza nchini Sudan zimekiinarisha kikosi hicho kuelekea michuano ya kimataifa.

Akizungumza na Spotileo, Meneja huyo ameeleza kuwa mechi hizo zimemsaidia pia kocha Zoran Maki kujua uwezo wa wachezaji wengine ambao hajawahi kuwatumia tangu wasajiliwe.

“Simba tunaishukuru klabu ya Al Hilal kwa mwaliko waliotupa ukweli wametusaidia kukiimarisha kikosi chetu,” amesema Rweyemamu.

Amesema anaamini kwa ushindani walioupata katika mechi mbili walizocheza Sudan wapo tayari kwa mashindano yote.

Ikiwa Sudan, Simba imecheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana na kushinda mabao 4-2 lakini ikapoteza mchezo wa pili dhidi ya wenyeji Al Hilal kwa bao 1-0.

Related Articles

Back to top button