
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo mitatu huku mchezo kivutio ukiwa kati ya Yanga na Coastal Union.
Mchezo huo wa mzunguko wa pili utafanyika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mchezo wa raundi ya kwanza kati ya timu hizo Yanga iliifunga Coastal mabao 2-0 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Agosti 20, 2022.
Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 41 baaa ya michezo 16 wakati Coastal ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 15 baada ya michezo 16.
Katika mchezo mwingine Ruvu Shooting ni mwenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mtibwa Sugar inashika nafasi ya 5 ikiwa na pointi 23 baada ya michezo 16 wakati Ruvu Shooting ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 11 baada ya michezo 16 pia.
Nayo Ihefu itakuwa mgeni wa Namungo kwenye uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi.
Namungo ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 19 baada ya michezo 16 wakati Ihefu ni ya 14 ikiwa na pointi 14 baada ya michezo 16.