Nyumbani

Ali Kamwe: Chama katuletea zaidi ya mashabiki 3,000

MSEMAJI wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe amesema mashabiki zaidi ya 3,000 wamehama pamoja na kiungo mpya wa timu hiyo Clatus Chama na kujiunga na Yanga na sasa wanaandaa utaratibu wa kuwapokea na kuwatangaza kuwa mashabiki wao wapya.

Kamwe amesema kati ya mashabiki hao waliohamia katika timu hiyo wakimfuata Chama baba yake mzazi ni miongoni mwao ingawa alimtaka asimtangaze kama amehamia Yanga.

“Baba yangu amesema kutokana na utu uzima wake, afya na mambo mengine, hayupo tayari kuendelea kujitesa na Simba amehamia Yanga ila ameniomba nisimtangaze ila mimi nimeshindwa kuvumilia nimemtangaza naye atakuwa miongoni mwa mashabiki tutakaowatangaza,” alisema.
Chama aliyesajiliwa mwaka mmoja na klabu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Simba.

Kamwe amesema licha ya faida hiyo pia Chama atasaidia Yanga kibiashara, kuanzia jezi na vitu mbalimbali vikiwemo makampuni mbalimbai kujitokeza kuwekeza kwa klabu hiyo.

Mchezaji kufuatwa na mashabiki ni kitu cha kawaida Roanaldo alivyohama kutoka Manchester United kujiunga na Real Madrid alihama na mashabiki wengi walimfuata kutokana na mapenzi ya mashabiki hao kwa Ronaldo, ndivyo ilivyokuwa kwa Chama na baadhi ya mashabiki wake.

Related Articles

Back to top button