
LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja mkoani Mbeya.
Mbeya City nimwenyeji wa Namungo katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Namungo inashika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 15 baada ya michezo 9 wakati Mbeya City ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 12 baada ya michezo 8.
Katika mchezo wa mwisho timu hizo kukutana ligi kuu katika uwanja wa Sokoine Juni 29, 2022 zilitoka sare ya bao 1-1