EPL
Maxenle Lacroix kuvaa jezi namba 23 Chelsea

LONDON: Beki mpya wa Chelsea, Maxence Lacroix, anatarajiwa kuvaa jezi namba 23 baada ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Stamford Bridge.
Namba hiyo ilikuwa ikivaliwa na Trevoh Chalobah, ambaye yupo karibu kukamilisha uhamisho wake kwenda klabu ya Como inayoshiriki Ligi Kuu Italia (Serie A).
Baada ya kuondoka kwa Chalobah, nafasi itafunguka kwa Lacroix kuanza maisha yake mapya Chelsea akiwa na jezi hiyo.
Taarifa kutoka kwa mwandishi maarufu wa masuala ya uhamisho, Fabrizio Romano, zilieleza kuwa Lacroix atavaa namba 23 mara tu uhamisho wake utakapokamilika rasmi.
Lacroix anatarajiwa kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi ya Chelsea baada ya kujijengea jina kama beki mwenye uwezo mkubwa akiwa na Crystal Palace.




