Matumaini ya kushinda ni makubwa-Mangungu


MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema ana imani kikosi hicho leo kitaanza na ushindi katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali kufuzu michuano ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets.
Akizungumza na Spotileo amesema licha ya kuwepo kwa changamoto za mwalimu lakini makocha waliopo wanasifa za kuipa ushindi timu hiyo.
“Matumaini ya kushinda dhidi ya Nyasa Big Bullets ni makubwa kutokana na ubora wa kikosi chetu lakini pia makocha ni wazuri wa mbinu hasa katika mechi hizo za mtoano,” amesema Mangungu.
Mwenyekiti huyo wa Simba kabla ya timu kuondoka nchini uongozi ulizungumza na wachezaji na kuwaeleza umuhimu wa mchezo huo hivyo anaamini watapambana kuhakikisha wanatimiza wajibu wao.
Simba itakuwa ugenini uwanja wa taifa Bingu uliopo jiji la Lilongwe kukabiliana na miamba ya soka ya Malawi, Nyasa Big Bullets.