EPL

Man U yatangaza bei ya Onana

MANCHESTER, Mashetani wekundu Manchester United wameweka wazi dau wanalolihitaji ikiwa kuna klabu inataka kumng’oa Golikipa wao namba moja Andre Onana kunako viunga vya Old Trafford.

Hatua hiyo ya Manchester united imetafsiriwa na mashabiki wengi wenye mahaba mazito naye kama kumchoka nyota huyo raia wa Cameroon na wapo tayari kuanza maisha mapya bila yeye.

Mashetani hao Wekundu wameeleza wanahitaji Pauni 30 milioni tu, katika dirisha hili kwa ajili ya kumuuza kipa wao, Andre Onana. Taarifa zikiongeza kuwa Kocha Ruben Amorim, haridhishwi na kiwango chake kikiambatana na makosa mengi binafsi yanayoigharimu timu hiyo mara nyingi.

Ripoti zinadai kuwa klabu ya AS Monaco ingetamani sana kupata huduma ya Onana lakini bei hiyo iliyowekwa na vigogo wa United inakuwa kikwazo kikubwa kwa klabu hiyo ya Ligue 1.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button