Nyumbani

Makonda awaonya viongozi wa michezo

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amewaonya viongozi wa mashirikisho ya michezo nchini wanaoshindwa kutekeleza ahadi walizozitoa kwa wanachama wao kuwa wako hatarini kung’olewa madarakani.

Makonda amesema ofisi yake itaanza kufuatilia utekelezaji wa ahadi hizo na endapo itabainika kuwa hazijafikia hata asilimia 20 ya yale waliyoahidi wakati wa uchaguzi, wizara itashirikiana na wanachama kuleta mabadiliko ya uongozi.

Akizungumza Dar es Salaam Leo katika mkutano wa Baraza la Michezo la Taifa uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Makonda amesema viongozi wengi waliingia madarakani kwa ahadi nyingi lakini utekelezaji wake ni mdogo.

“Nyinyi mlipata nafasi hizi kwa kupigiwa kura na wanachama wenu. Ni lazima mujiulize mmetimiza kwa kiwango gani ahadi mlizotoa kwa waliowachagua,” amesema.

Amesema kuwa serikali haitaridhika kuona viongozi wanaendelea kushikilia madaraka bila kuonesha matokeo katika maendeleo ya michezo.

Makonda ameongeza kuwa amepewa jukumu la kuhakikisha sekta ya michezo inaleta matokeo kwa taifa, hivyo viongozi wa mashirikisho wanapaswa kuwajibika kwa wanachama na kwa maendeleo ya michezo nchini.

Aidha aliwataka viongozi hao kuimarisha uwazi katika uendeshaji wa mas hirikisho yao na kushughulikia migogoro ya ndani inayokwamisha maendeleo ya michezo.

Related Articles

Back to top button