Ligi KuuNyumbani

Makata hajakata tamaa Ruvu Shooting

KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting, Mbwana Makata amesema atatumia uwezo na mbinu zake zote kuhakikisha timu hiyo haishuki daraja msimu huu.

Ruvu ikicheza uwanja wa Azam Complex Desemba 16 imepokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Ihefu huku mchezi huo ukiwa wa kwanza kwa Makata tangu alipoteuliwa kuwa kocha wa Ruvu.

Akizungumza na SpotiLeo, kocha huyo amesema kuhakikisha hilo linatimia amepanga kukutana na uongozi wa juu ili kukiboresha kikosi cha timu hiyo kupitia usajili wa dirisha dogo.

“Ni kweli hatupo kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo lakini hiyo haimaamishi kwamba tutashuka daraja bado nina imani kubwa na timu hii nitahakikisha inarudi kwenye ushindani,” amesema Makata.

Kocha huyo aliyeteuliwa kukinoa kikosi cha Ruvu hivi karibuni amesema kuna mapungufu katika nafasi za ulinzi, kiungo na hata ushambuliaji na anaamini uongozi wa timu hiyo utampa ushirikiano katika maboresho anayokusudia kuyafanya.

Ruvu Shooting ipo nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 11 baada ya mchezo 16.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button