World Cup

Majeruhi Mane aitwa kikosi cha Senegal

MSHAMBULIAJI Sadio Mane wa Bayern Munich ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Senegal ‘Simba wa Teranga’ kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2022 licha ya kupata majeraha wakati wa mchezo wa Bundesliga dhidi ya Werder Bremen Novemba 8.

Katika mchezo huo wa mwisho wa Bayern kabla ya Kombe la Dunia iliposhinda mabao 6-1 Mane aliondolewa uwanjani Allianz baada ya dakika 21 tu tangu mpira kuanza alipoonekana kuumia mguu.

Senegal itaanza kampeni ya Kombe la Dunia Novemba 21 dhidi ya Uholanzi kundi A na Mane atakuwa muhimu katika matumaini ya nchi hiyo kufuzu 16 bora katika kundi hilo linalojumuisha pia wenyeji Qatar na Ecuador.

Kikosi kamili cha Senegal kwa ajili ya Kombe la Dunia ni kama ifuatavyo:

Magolikipa: Edouard Mendy, Alfred Gomis na Seny Diang

Walinzi: Kalidou Koulibaly, Pape Abou Cisse, Abdou Diallo, Fode Ballo Toure, Youssouf Sabaly, Ismail Jakobs na Formose Mendy.

Viungo: Pape Matar Sarr, Pape Gueye, Nampalys Mendy, Idrissa Gana Gueye, Moustapha Name, Loum Ndiaye, Cheikhou Kouyate, Krepin Diatta na Pathe Ciss.

Washambuliaji: Sadio Mane, Ismaila Sarr, Bamba Dieng, Boulaye Dia, Famara Diedhiou, Ilman Ndiaye na Nicolas Jackson.

Related Articles

Back to top button