EPL

Majeraha ya Eliott yamvuruga Slot

KIUNGO wa klabu ya Liverpool Harvey Eliott anakabiliwa na wiki kadhaa za kuwa nje ya uwanja baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu akiwa katika majukumu yake ya timu ya taifa.

Nyota huyo anaekipiga katika timu ya vijana wa umri chini ya miaka 21 alipata majeraha hayo wakati timu ya England U21 ilipokuwa ikijiandaa na michezo miwili dhidi ya Northern Ireland na Austria.

Kuumia kwa kinda huyo kunampa wakati mgumu kocha wa kikosi cha Liverpool Arne slot ambaye bado yupo kwenye tafakari nzito ya utimamu wa viungo Curtis Jones na Alexis Mac Allister kuelekea mchezo wao dhidi ya Nottingham Forest, Jumamosi Septemba 14.

Kwa mujibu wa jarida la The times la nchini England kinda huyo atakuwa nje kwa wiki sita japo Liverpool bado hawajathibitisha.

Eliott anaungana na nyota kama Martin Odegard wa Arsenal na Nathan Ake wa Manchester city ambao pia wanaouguza majeraha kutokana na kuzitumikia timu zao za taifa.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button