Tetesi

Mac Allister kufanyiwa vipimo Liverpool leo

BAADA ya uhakika wa usajili wa Alexis Mac Allister, kutoka Brighton, Liverpool imeomba kumfanyia vipimo vya afya kiungo huyo raia Argentina leo.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wa habari za michezo, Fabrizio Romano amesema kiungo huyo atasaini mkataba wa miaka mitano kesho.

Ameeleza kuwa Mac Allister anataka usajili huo ukamilike kabla ya kurudi Argentina.

Baada ya usajili huo, Liverpool pia inahusishwa na wachezaji Manu Koné, Borrusia Monchengladbach na Khephren Thuram kutoka Nice.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button