Tetesi

Tetesi za usajili

BEKI wa kati wa Nice, Jean-Clair Todibo anakaribia kuhamia Manchester United licha ya hofu uhamisho unaweza kukwama baada ya jaribio la uhamisho wa Harry Maguire kwenda West Ham United kuingia mchanga. (L’Equipe)

Liverpool imeona chungu ya ofa yake ya pauni milioni 25.5 kumsajili kiungo wa Fluminense Andre kukataliwa na klabu hiyo haitarajiwi kuongeza dau.(ESPN)

Bayern Munich imetuma ombi la kumsajili beki wa kati wa Southampton, Armel Bella-Kotchap ambaye pia ameivutia Borussia Dortmund.(Florian Plettenberg)

Huenda kiungo Ryan Gravenberch akaondoka Bayern. Mdachi huyo anahitajika Man Utd na Liverpool lakini Galatasaray imetoa ofa ya ada ya mkopo pauni milioni 8.5 na chaguo la dili la kudumu la pauni milioni 17.(Burhan Can Terzi)

Fiorentina imemonya kiungo Sofyan Amrabat kwamba hadi Agosti 25 awe amefanya maamuzi ya mwisho kuhusu hatma yake katika klabu hiyo kufuatia Man Utd, Liverpool na Atletico Madrid kuonesha nia kumsajili. (Corriere dello Sport)

Barcelona ina mpango wa kushindana na Real Madrid na Manchester City majira yajayo ya kiangazi kupata saini ya kiungo wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz anayekadiriwa kugharimu pauni milioni 85.5. (SPORT)

Mwaka 2024 pia unaweza kushuhudia hatimaye Real Madrid ikichochea uhamisho wa beki wa kushoto wa Bayern Munich, Alphonso Davies, ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 42.5.(Fichajes)

Tottenham itafikiria ofa kutoka nje kumsajili Eric Dier kufuatia nia kutoka Fulham, ambayo inajiandaa kumpoteza Tosin Adarabioyo kabla dirisha la usajili na uhamisho kufungwa.(Mail)

Related Articles

Back to top button