Tetesi

Bayern yamwinda Robertson

TETESI za usajili zinasema beki wa kushoto wa Liverpool na Scotland, Andy Robertson, 29, ni chaguo namba moja la usajili la mabingwa wa Ujerumani Bayern München wakati ikipanga namna ya kuziba pengo la mchezaji wa kimataifa wa Canada, Alphonso Davies, ambaye anatarajiwa kujiunga na Real Madrid. (Daily Mail)

Wasiwasi wa Arsenal kuhusu rekodi ya majeraha ya mshambuliaji wa Brazil, Gabriel Jesus ni sababu ya kusaka mshambuliaji mpya huku Ivan Toney wa Brentford, Victor Osimhen wa Napoli, Joshua Zirkzee wa Bologna na Viktor Gyokeres toka Sporting miongoni mwa machaguo. (Daily Mail)

Arsenal ina nia kumsajili beki wa Ajax, Jorrel Hato, 17, lakini klabu hiyo ya kidachi ina matumaini kumfunga kwa mkataba mpya. (Evening Standard)

Barcelona inafikiria kumsajili golikipa wa zamani wa Manchester United, David de Gea, 33, huku mhispania huyo sasa akiwa mchezaji huru. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Newcastle United na Tottenham zina nia kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Misri na Eintracht Frankfurt, Omar Marmoush, 25, ambaye amefunga mabao 10 katika michezo 18 ya Ligi Kuu Ujerumani, Bundesliga msimu huu. (Bild via Shields Gazette)

Related Articles

Back to top button