Lulu ampongeza mumewe kwa ujumbe ‘spesho’ wa birthday

DAR ES SALAAM:MSANII maarufu kutoka tasnia ya filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amemimina maneno ya mapenzi na pongezi kwa mumewe Francis Siza ‘Majizo’ katika maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa katika ujumbe mzito aliouandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Lulu ameeleza kuwa Majizo ni jibu la sala zake, akimsifu si tu kama mume na baba, bali pia rafiki, mshirika wa biashara, na nguzo muhimu katika maisha yake.
Katika sehemu ya ujumbe huo ameandika:Happy birthday Muhimili wetu mkuu (mtaelewa kwenye last slide). Kwa lugha rahisi tu, wewe ni sala zangu zilijobiwa. Mwenyezi Mungu akuongezee umri uliojaa mema ya rohoni na mwilini.
Ameendelea kwa kusema:Ahsante kwa kuwa Baba, Mume, Rafiki, Business Partner, Mubaba, Danga… au skia, wewe ni Mihamala yote bwana na hatuwezi kuingilia Mihamala yako yote. Ishi sana Role Model… Nakupenda Mume wangu Majizo.
Ujumbe huu wa Lulu umeibua hisia mseto mitandaoni, ambapo wengi wameonesha kuguswa na uhusiano wao wa karibu na wa kuheshimiana.




