“Liwalo na liwe!” – Maresca

LONDON: KOCHA wa Chelsea Enzo Maresca amesema hakuwa akihisi shinikizo lolote la ziada katika kipindi hiki ambacho klabu yake ipo katika siku tatu za maamuzi ambapo kikosi chake kitajaribu kujihakikishia nafasi moja kati ya tatu zilizosalia za Ligi Ya Mabingwa katika timu tano bora za Premier League, kabla ya kukabiliana na Real Betis katika fainali ya UEFA Conference League.
Chelsea walio kwenye nafasi ya tano watakuwa wageni wa Nottingham Forest wenye nafasi ya saba jumapili hii mchezo amba oni wa mwisho kwa msimu wa 2024/25, ambapo gepu la pointi baina yao ni moja pekee kabla ya kupaa kwenda Poland kwa fainali ya Conference League dhidi ya Real Betis Jumatano.
“’Presha ipo kila siku, nimekuwa na presha tangu nilipojiunga klabuni hapa kwa sababu hapa unahitaji kushinda kila mchezo. Huu ni Ushahidi tosha kuwa ligi hii ni ngumu timu thabiti ni Liverpool pekee, ndio maana ni mabingwa wengine walikuwa na panda shuka nyingi msimu huu ” Maresca aliambia waandishi habari.
Vijana wa Maresca bado wana nafasi ya kumaliza katika nafasi tatu za juu, iwapo watashinda mchezo wao wa mwisho huku wakiomba dua mbaya kwa Manchester City walio nafasi ya tatu na tofauti ya pointi kati yao zikiwa 2 pekee lakini kipigo au sare haitakuwa chaguo lao.
Chelsea inaweza kupata nguvu kwa urejeo wa washambuliaji Christopher Nkunku na Marc Guiu waliopona majeraha ya muda mrefu, lakini Nottingham Forest bado ni mtihani mgumu kwa Maresca kwani na wao wanaitafuta nafasi hiyo ya Ligi Ya Mabingwa msimu ujao.