Kwingineko

Atletico Madrid kupindua meza UCL leo?

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya(UCL) hatua ya 16 bora inaendelea leo kwa michezo miwili ya marudiano itakayopigwa Hispania na Ujerumani.

Baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 toka kwa Inter katika mchezo wa kwanza, Atletico de Madrid itakuwa uwanja wa nyumbani wa Civitas Metropolitano jijini Madrid ikitaka kupindua meza ili kufuzu robo fainali.

PSV Eindhoven itakuwa ugenini kuivaa Borussia Dortmund kwenye uwanja wa
Signal Iduna Park jijini Dortmund.

Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kwanza.

Related Articles

Back to top button