Mastaa

Linah Sanga: “Sitamani ndoa kwa sasa”

DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Fleva, Linah Sanga, amesema kwa sasa hana kabisa shauku ya kuingia kwenye ndoa, na kwamba anahitaji muda wa kupumzika na kufurahia ujana wake.

Amesema hayo ikiwa ni miaka michache tangu kutangaza kuachana na baba wa mtoto wake, ambaye pia aliwahi kuwa meneja wake katika kazi zake za muziki.

Linah amefafanua kuwa, ingawa anatamani kuwa na mwanaume mwenye mapenzi ya dhati, anayejali na mwenye kujituma, bado hajaweka kipaumbele kwenye suala la ndoa.

“Natamani sana kupata mwanaume mwenye mapenzi, matunzo na anayejali sana. Sitamani hata kuolewa kwa sasa, nataka nichill tu kwanza, nile mema ya dunia,” amesema Linah Sanga.

Tangu kuachana na baba wa mtoto wake, Linah amekuwa akihusishwa mara kwa mara na wanaume mbalimbali, ingawa yeye mara nyingi amekuwa akikwepa kuzungumzia uvumi

Related Articles

Back to top button