Ligi Ya WanawakeNyumbani
Ligi Kuu wanawake kuanza leo
LIGI Kuu ya mpira wa miguu ya wanawake msimu wa 2023/2024 inaanza leo kwa michezo minne ya ufunguzi kwenye viwanja tofauti.
Mabingwa watetezi JKT Queens itaanza kampeni kutetea taji hilo ugenini dhidi ya Bunda Queens kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma mkoa wa Mara.
Simba Queens itaikaribisha Ceasiaa Queens kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Geita Gold Queens itakuwa mgeni wa Alliance Girls kwenye uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza.
Washindi wa nne wa Ngao ya Jamii wanawake 2023, Fountain Gate Princess itaikaribisha Amani Queens kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.




