KwinginekoSerie A

Lecce yamsajili Umtiti kwa mkopo

KLABU ya Barcelona imethibitisha kuwa beki wake Samwel Umtiti amejiunga na Unione Sportiva Lecce ya Italia kwa mkopo wa msimu mzima.

Imeripotiwa kuwa Lecce itailipa Barcelona ada itakayotofautina kutegemea kiwango atakachokionesha Umtiti msimu huu.

Alisaini Barcelona 2016 akitokea Lyon kwa mkataba wa Euro milioni 25 sawa na shilingi bilioni 57,559,807,500 na kucheza michezo 133 klabu hiyo ya Catalan.

Mapema mwaka huu Umtiti mwenye umri wa miaka 28 alisaini mkataba mpya Barca hadi 2026.

Lecce ilimaliza kinara katika ligi ya Serie B msimu uliopita hivyo kurejea Ligi kuu ya Italia, Serie A.

Related Articles

Back to top button