Ligi Kuu

Kwa kauli hizi! baaasi kuna nini tena?

Kocha Yanga aingia na mkakati mpya

KIGOMA: KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Hamdi Miloud kinashuka dimbani kesho kusaka alama tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mashujaa FC.

Yanga watakuwa ugenini katika mchezo huo utakaochezwa katika dimba la Lake Tanganyika, mkoani humo kila timu ikihitaji alama tatu ili kufikia malengo yao kwa wananchi kuendelea kujiimarisha katika uongozi wa ligi hiyo, Mashujaa FC wakihitaji kujiweka salama kutoshuka daraja.

Kuelekea mchezo huo Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud amesema wanaheshimu timu hiyo wanaweza kucheza vizuri sana wana wachezaji wengi wazuri, anafikiri wanaweza kuwa juu zaidi kwenye ligi, anajua kila timu inataka kufanya kila kitu kushida dhidi yao.

“Wachezaji wetu wanajua hilo, tunapaswa kufanya kila kitu kutumia jitihada nyingi kushinda mchezo huu. Ni jambo jema kuwa na siku tano kabla ya mchezo huu, nafasi nzuri kwangu kuelewa wachezaji wangu vizuri zaidi,” amesema.

Miloud amesema amepata muda wa kufanya marekebisho ya kiufundi mazoezini, kuweka mtazamano wake kidogo kwa sababu si rahisi kubadilisha kila kitu mara moja, wachezaji wana tabia zao za uchezaji sio rahisi kubadilisha kila kitu.

Related Articles

Back to top button