Kuogelea

Kuogelea kuwakilisha nchi michuano ya Afrika

DAR ES SALAAM:TIMU ya Taifa ya Kuogelea inatarajiwa kuondoka kesho kuelekea nchini Misri kushiriki mashindano ya vijana ya Afrika huku Baraza la Michezo la Taifa BMT likiwakabidhi bendera na kuwataka wakafanye vizuri.

Akizungumza Dar es Salaam Leo wakati wa kukabidhi bendera, Ofisa Michezo wa BMT Charles Maguzu amesema Watanzania wawaombee ili warudi na vikombe na medali.

“Tunawapongeza wote waliochaguliwa kuwakilisha timu ya Taifa.Msimuogooe mtu, chukueni bendera mkaipiganie na sisi tutawasubiri kuwapokea mkija na vikombe na medali,”amesema.

Mwenyekiti wa Chama cha Kuogelea Tanzania TSA David Mwasyoge amesema anaamini kikosi kinachokwenda kitafanya vizuri na kuwatakia kila la heri katika mashindano hayo.

Nahodha wa timu hiyo Romeo Mwaipasi amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaendelea kuvunja rekodi mbalimbali za kitaifa na kurudi na ushindi.

Wachezaji wanaokwenda ni pamoja na Bridget Heep, Aminaz Kachra atashiriki na Aliyana Kachra na kwa upande wa wavulana Christian Fernandes na Romeo.

Related Articles

Back to top button