Habari MpyaNyumbani

Kocha amemsamehe, adhabu ya uongozi pale pale

DAR ES SALAAM: MENEJA wa Idara ya habari na mawasiliana wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa mshambuliaji wao, Kibu Denis amesamehewa na Kocha Fadlu Davids lakini adhabu ya uongozi ipo pale pale.

Denis, amejiunga na Simba kwa ajili ya mazoezi baada ya kutatua tatizo la awali kuhusu kuchelewa kujiunga kutokana na majaribio nchini Norway, hali iliyozua wasiwasi, lakini sasa amejiunga tena na timu hiyo.

Ahmed amesema walitarajia kuna muda mshambuliaji wao atarejea kikosini na amezungumza na kocha Fadlu baada ya kuridhika nyota huyo kuingia kambini kuendelea na majukumu yake ya kutumikia mkataba wake wa miaka miwili.

“Ni kweli kocha amemsamehe Kibu lakini bado uongozi wa ngazi ya juu haujatoa adhabu, atambue lazima achukuliwe hatua ili kukomesha jambo la utovu wa nidhamu ambao ameufanya,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa adhabu hiyo ni kutofuata utaratibu wa kuondoka nchini na kwenda Norway bila kuaga waajiri wake na itakuwa fundisho kwa wachezaji wengine wenye fikra za kutaka kufanya alivyofanya Kibu.

“Mchezaji yeyote anayefuata malisho mema kutoka nje ya Tanzania anatakiwa kufuata utaratibu kwa sababu Simba haina utamaduni wa kuzuia mchezaji, ikumbukwe kuna kipindi ilimuuza mshambuliaji wake Emmanuel Okwi, tuliumia lakini hatukujali,” amesema Meneja wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button