Ligi Ya WanawakeNyumbani

Kocha aahidi makubwa Mkwawa Queens

KOCHA Mkuu wa Mkwawa Queens, Miraji Fundi ameahidi kupambana ili kuisaidia timu yake ibaki katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara.

Fundi amesema hayo wakati wa mahojiano malumu na gazeti la HabariLEO.

Amesema timu hiyo haipo katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo, ila ana amini wakipambana watasalia kubaki.

Amesema bado mechi ni nyingi sana hivyo watapambana kushinda na kusalia katika Ligi Kuu.

Amesema kwa sasa timu yake inaendelea vizuri na mazoezi katika Uwanja wa Mkwawa ili
kuiboresha katika maeneo tofauti.

Kocha huyo wa zamani wa Panama Queens na Baobab Queens amewaomba wadau na wapenzi wa soka mkoani Iringa waendelee kuisaidia timu yao iweze kufanya vyema katika ligi hiyo.

Kiungo wa Mkwawa Queens, Herieth Edward amesema watapambana ili kushinda michezo iliyopo mbele yao.

Katika msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake Mkwawa Queens ipo mkiani ikiwa na pointi
moja baada ya michezo sita iliyocheza mpaka sasa.

Timu hiyo imepata sare moja na kupoteza mechi tano. Mkwawa imefunga bao moja na
imefungwa mabao 13.

Related Articles

Back to top button