FANyumbani

Kivumbi raundi ya kwanza FA

MICHUANO ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC)-FA raundi ya kwanza inaendelea leo kwa michezo 15 katika viwanja tofauti.

Usalama itavaana na New Dundee katika uwanja wa Fountain Gate, Dodoma wakati Ifunda itavurumishana na Lipuli katika uwanja wa Sokoine, Iringa.

Zamalek itakutana na Mbeya Road katika uwanja wa Sabasaba, Njombe wakati Majimaji itakwaana na Mbuga katika uwanja wa Majimaji, Ruvuma.

Stand na Sodeco zitamenyana katika uwanja wa Boma, Mtwara wakati Eagle itakuwa ikipepetana na Navy katika uwanja wa Air Wing, Dar es Salaam.

Nazo Katesh Cluster na Misitu zitapambana katika uwanja wa Shule ya Sekondari Singe, Manyara.

Moto utawaka katika uwanja wa Lake Tanganyika wakati Kigoma Kwanza itakapokuwa kazini dhidi ya Kasulu, mkoani Kigoma huku Gold City ikionyeshana kazi na Nzega United katika uwanja wa Nyankumbu, Geita.

Itobo Rangers na Buhaya zitatimua vumbi katika uwanja wa Sabasaba, Tabora wakati Greenland itapambana na Rhino Rangers katika uwanja wa Kaitaba, Kagera.

Nyasi za uwanja wa Karume mkoani Mara zitawaka moto wakati Buhare itakapoikabili Vijana huku Moro Kids ikivaana na Silent Ocean katika uwanja wa jamhuri, Morogoro.

Polisi Katavi itakuwa dimbani dhidi ya Tunduma City katika uwanja wa Azimio, Katavi wakati Ndunguti itakiwasha na Singida Cluster katika uwanja wa Ndunguti, Singida.

Related Articles

Back to top button