World Cup
		
	
	
Kivumbi kukamilisha makundi kombe la dunia
						MICHEZO ya kukamilisha mechi za makundi katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea Qatar inaanza leo.
Katika Kundi A wawakilishi wa Afrika Senegal itakamilisha mechi za makundi kwa kupambana na Ecuador wakati wenyeji wa michuano hiyo ambayo tayari imeondolewa Qatar itapambana na Uholanzi.
Kundi B litashuhudia Iran ikipambana na Marekani wakati England itavaana na Wales.
Brazil, Ufaransa na Ureno tayari zimefuzu hatua ya 16 bora.
				
					



