
MECHI mbili za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 zinapigwa leo huku Tanzania ikicheza dhidi ya Uganda Machi 24 kwenye dimba la Suez Canal, Ismailia, Misri.

Mchezo wa marudiano kati ya Taifa Stars na Uganda Cranes zilizopo kundi F utafanyika Machi 28 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mechi zinazopigwa leo Siera Leone itakuwa mwenye wa Sao Tome and Principe kundi A wakati Rwanda ipo ugegeni kuivaa Benin katika kundi L.