
TIMU ya taifa ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ jumapili hii Juni 18, 2023, itacheza mchezo uliobeba hatma ya kufuzu kucheza michuano ya Afcon mwaka 2023 nchini Ivory Coast.
Taifa Stars inashika nafasi ya pili kwenye kundi F ikiwa na alama nne baada ya michezo Minne, itashuka dimbani dhidi ya Niger katika mchezo wa tano wa kundi hilo uliobeba matumaini ya timu hiyo.
Tayari kikosi cha Stars kipo kambini kikijiwinda na mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa siku ya jumapili.
Mpaka sasa Algeria wanaongoza Kundi F wakiwa na alama 12, Tanzania inashika nafasi ya pili ikiwa na alama nne, Uganda nafasi ya tatu akiwa na alama nne huku Niger wakiburuza mkia na alama zao mbili.