Kikapu Dar kutimua vumbi Mei 3

DAR ES SALAAM:LIGI ya kikapu mkoa wa Dar es Salaam inatarajiwa kutimua vumbi Mei 3, mwaka huu na kushirikisha timu 32 za wanaume na wanawake.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Ufundi na Mashindano wa Chama cha Kikapu mkoa wa Dar es Salaam Haleluya Kavalambi, wanategemea ushindani zaidi msimu huu kushinda mwaka jana.
Kavalambi amehimiza timu kufanya maandalizi mazuri kuhakikisha zinakuja kiushindani. Msimu uliopita bingwa alikuwa JKT aliyemfunga UDSM Outsiders katika mchezo wa fainali.
Timu zinazotarajiwa kuchuana msimu huu kwa wanaume ni ABC, Chui, Dar City, Donbosco Oratory, JKT, Kampala University, Kurasini heat, Mchenga, Mgulani, Pazi, Polisi,Savio, Srelio, Stein, UDSM Outsiders na Vijana.
Kwa upande wa wanawake pia, kutakuwa na timu 16 ambazo ni City Queens, Don Bosco Lioness, Troncatti, Jeshi Stars, Kigamboni Queens, Kurasini Divas, Mgulani Stars, Polisi Stars, Reel Dream, Tausi, Twalipo, UDSM Queens, Ukonga Queens na Vijana Queens.