Kwingineko

Kifo cha mama kilimuingiza Dutt kwenye dawa za kulevya

MUMBAI: DADA wa Sanjay Dutt. Priya Dutt amesema hakuna vituo vya kurekebisha tabia ambavyo vinaweza kumsaidia mwigizaji huyo na uraibu wa dawa za kulevya hadi siku moja aliposikia sauti kutoka kwa mama yake mzazi Nargis.

Kifo cha Nargis Dutt kiliacha athari kubwa kwa Sanjay Dutt, ambaye akiwa na miaka 21 tu wakati huo alikuwa muigizaji tayari lakini ndugu zake waliishi New York Marekani akiwemo baba yake na dada zake.

Wakati huu, Sanjay aliingia katika uraibu wa dawa za kulevya, ambayo ilipoteza miaka kadhaa ya maisha yake kutembelea rehabs. Muigizaji huyo pia alikuwa na huzuni kwani hakuweza kutimiza matakwa ya mwisho ya mama yake ya kumuonesha filamu yake ya kwanza.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na Vickey Lalwani, dada mdogo wa Sanjay Dutt, Priya Dutt, alikumbuka wakati wa 1980-81 ambao ulibadilisha maisha yao milele kwani wao wakiwa ulaya Sanjaya likuwa ashaingia katika dawa za kulevya nchini india.

“Kwa kuwa alikuwa hapa (India) muda mwingi. Hakuna mtu aliyekuwa na muda wa kumjulia hali, kwa sababu lengo letu wakati huo lilikuwa mama yetu na ugonjwa wake tukamsahau Sanjay hadi mama alipofariki mambo yakawa mabaya zaidia kwa muigizaji huyo.”

“Kufariki kwa mama kulimletea madhara makubwa sana.” Nargis, ambaye alikuwa mgonjwa, alitaka mwanawe atoe filamu yake ya kwanza bila kuchelewa. Ili kumtia motisha nyota huyo wa sasa, Nargis aliahidi kuwa hapo kwa ajili ya onesho la kwanza la filamu hiyo hata ikiwa atalazimika kuja kwa machela.”

“Hii ilikuwa ngumu sana kwake kwamba hakuweza kuona filamu yake ya kwanza. Onesho la kwanza la Rocky lilifanyika na tuliweka kiti tupu kwa mama karibu na baba,” alisema Priya. Filamu hiyo ilifanya vizuri lakini Mama yetu hakuishihudia kama alivyotamani wala fedha nyingi alizopata Sanjay Dutt, katika uzinduzi huo hazikuwa na maana yoyote kwakekwani mama yake hakuona kazi yake.

Hali hiyo ilimrudisha tena katika matumizi ya dawa za kulevya na hakuna aliyeweza kumsaidia zaidia ya kumuhamisha katika vituo mbalimbali vya matibabu ya watu wanaotumia dawa za kulevya.

Related Articles

Back to top button