Karate Kid Legends ya Jackie Chan yakosolewa

NEW YORK: WAKOSOAJI wa filamu wameikosoa filamu ya Karate Kid Legends iliyoshirikisha wakali wa filamu za mapigano Jackie Chan na Ralpha Macchio kwamba haina jipya matukio ni yale yale kwenye filamu ya awali.
Wakosoaji hao wameikosoa filamu hiyo wakati wa utazaji wa awali kabla haijapelekwa kwenye majimba ya sinema.
Wakosoaji hao wamesema wakali Jackie Chan na Ralph Macchio wamesimamia vyema ukufunzi wa mapigano katika filamu hiyo lakini hadithi na mtiririko wa matukio yake hautofautiani na filamu ya awali.
Hadithi ya filamu hiyo iliyoongozwa na Jonathan Entwistle ni hadithi ya mtoto ambaye anaonewa na lazima apambane na wavulana wenye nguvu kuliko yeye.
Katika mchakato huo, hukutana na mzee mwenye busara hujifunza namna ya kupigana na hatimaye anajua.
“Hivi ndivyo kila filamu ya Karate Kid imekuwa kwa miaka 40 iliyopita. Kinachofanya Legends kuchosha ni kwamba si tu kwamba unajua kitakachotokea, unaweza kutabiri kwa usahihi jinsi kitakachotokea hadi wanachozungumza. Inatabirika sana,” wameeleza.
Kabla ya hadithi kuanza, urejeleaji kidogo wa franchise hutuambia jinsi karate ya Miyagi inavyounganishwa na shule ya Han ya kung fu nchini Uchina.