Ligi KuuNyumbani

Kagera Sugar yamtupia virago Makame

KLABU ya Kagera Sugar imetangaza kuvunja mkataba na mchezaje wake Abdul Aziz Makame.

Taarifa ya Kagera Sugar haijaeleza sababu za kuvunja mkataba na Makame na imemshukuru kwa huduma yake katika muda wa mwaka mmoja akiitumikia timu hiyo.

“Klabu ya Kagera Sugar tunapenda kuujulisha umma na wanamichezo wote kwamba leo tar 4 April 2023 tumefikia makubaliano ya kuvunja mkabata na aliyekuwa mchezaji wetu ABDUL AZIZ MAKAME,” imesema taarifa hiyo.

Makame alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Kagera Sugar Julai 2022.

Related Articles

Back to top button