Ligi KuuNyumbani

Kagera Sugar kuizuia Simba?

BAADA ya ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold klabu ya Simba itashuka kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Agosti 20 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa mzungunzo wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema lengo ni kuhakikisha timu hiyo inapata ushindi ili kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi.

Matola amesema anajua mchezo utakuwa mgumu kutokana na historia ya wapinzani wao Kagera kuwa na timu nzuri ya ushindani lakini Simba imejidhatiti kuhakikisha inashinda.

“Ni mchezo mgumu tunawaheshimu Kagera Sugar kutokana na rekodi zao lakini kwa kutumia ubora wa kikosi chetu naamini tutashinda,” amesema Matola.

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Francis Baraza

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Francis Baraza amesema wamejiandaa vizuri kucheza na Simba ingawa anaamini utakuwa mchezo mgumu.

“Sisi Kagera tutakwenda kupambana bila hofu na kama watu hawaijui Kagera waangalie mchezo tuliocheza na Azam,” amesema Baraza.

Related Articles

Back to top button