Juve, Porto ni mali kwa mali

PORTO: IMEFAHAMIKA kuwa beki wa kulia wa Juventus Alberto Costa atajiunga na wababe wa Ureno FC Porto huku winga João Mário wa klabu hiyo akijiunga na Juventus katika kile kinachotajwa kama makubaliano ya kubadilishana wachezaji ambayo ni ya uhakika hata kama yatahusisha pesa za ziada na hii ni kwa mujibu wa mwanahabari wa Italia Fabrizio Romano
FC Porto watalipa Euro milioni 15 kukiwa na uwezekano wa nyongeza ya Euro milioni 1 kutegemeana na mafanikio ya malengo ya kumsajili Alberto Costa ambaye anatarajiwa kuwasili Ureno siku za usoni kukamilisha dili hilo huku klabu yake ya zamani ya Vitória SC ikipokea Euro laki moja na elfu 25.
Alberto Costa anajiandaa kurejea katika soka la Ureno baada ya kuondoka Vitória SC mwezi Januari akitumia miezi sita pekee nchini Italia. Wakati huo huo João Mário yuko njiani kuelekea Juventus kwa dili la thamani ya Euro milioni 12. Beki huyo wa pembeni aliyefanya mazoezi FC Porto anapiga hatua ya kwanza katika maisha yake ya soka la kimataifa.
Kwa hivyo, kwa kuzingatia hesabu za mwisho katika mikataba hii miwili FC Porto maarufu kwa jina la utani la ‘Dragons’ italipa euro milioni tatu pamoja na bonasi kunasa kusaini ya Alberto Costa na itamwachilia João Mário Kwenda Juve.