Ligi KuuNyumbani

Julio “Mungu ndiye anayegawa Riziki”

KOCHA wa KMC Jamhuri Kiwhelo Julio amesema matamanio yake ni kuijenga timu imara ya KMC kuelekea msimu ujao baada ya kufanikiwa kuibakisha timu hiyo ligi kuu.

Julio amesema Uongozi wa KMC ulitaka kumpa kandarasi ya miaka miwili lakini yeye aliwakatalia akitaka kuibakisha timu kwanza kisha taratibu nyingine zitafuata.

Kuhusu kama ataendelea kuwepo kwenye kikosi hicho Julio amesema itategema na Mipango ya Uongozi juu ya ni nani anafaa kukisuka kikosi hicho kwa msimu ujao.

” Tumeanza Mazungumzo ya mimi na wao ili kubaki kwenye timu lakini pia kufanya usajili,

“Nina imani nitabaki na KMC lakini hata kama wakiona kuna kocha mwingine mwenye uzoefu mimi sina shida kwasababu Mungu ndiye anayegawa Riziki”, amesema Julio

Julio alijiunga na KMC mwishoni mwa msimu uliomalizika na kufanikiwa kuinusuru timu hiyo na jinamizi la kushuka daraja.

Related Articles

Back to top button