Habari Mpya

JKT Queens, Kenya Elite Jr watafutana GIFT

DAR ES SALAAM: KIKOSI cha timu ya JKT Queens kesho kitashuka dimbani kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Kenya Elite Junior katika Mashindano ya CAF  U17 Girls  Integrated Football Tournament (GIFT) yanayoendelea katika Uwanja wa Azam Complex Dar Es Salaam.

Timu hizo zitashuka dimbani kila moja ikiwa imepata ushindi katika mchezo yao ya kwanza ambapo JKT Queens ilishinda mabao 3-0 dhidi ya K.A.S ya Kenya, wakati Kenya Elite Junior iliibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya City Lights Football ya Sudan Kusini.

Michuano hiyo ya GIFT inaendelea katika uwanja wa Azam Complex na Tanzania ikiwa nchi mwenyeji ikiwakilishwa na timu mbili, JKT Queens ikinolewa na Kocha Ester Chambruma na TDS chini ya kocha Hilda Masanche.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button