Mastaa

Jaya Bachchan awatibua wapiga picha

MUMBAI: MMOJA wa waigizaji wakongwe wa Bollywood, Jaya Bachchan amejikuta kwenye ugonvi na wapiga picha maarufu Paparazi baada ya kusema maneno makali kuhusu wao.

Alizungumza na mwandishi wa habari, Barkha Dutt, ambapo aliulizwa kuhusu uhusiano wake na paparazzi. Jaya alijibu kwa kusema hana uhusiano wowote na wapiga picha.

“Mimi ni sehemu ya vyombo vya habari. Nani hawa watu? Je, Unawaita vyombo vya habari? Mimi natoka kwenye vyombo vya habari. Baba yangu alikuwa mwandishi wa habari. Nina heshima kubwa kwa watu kama hao.”

Jaya aliendelea, “Lakini hawa watu, wanavaa masuluali manene kama mafundi bomba, wanavaa mavazi machafu, wao wanajua kushika simu na kupiga picha watu huku wakijiamulia cha kuandika! Wanatoka wapi? Wana elimu gani? Wana historia gani?” Maneno haya yaliibua hisia tofauti miongoni mwa paparazzi na wananchi waliokasirika na kauli ya Jaya.

Paparazzi waliitikia kwa hasira, wakisema kuwa wanahudumia kazi yao kwa uadilifu na hawahitaji kuoneshwa ubaguzi wa kijamii au kuonekana kama watu wabaya kwa sababu ya kazi yao. Walisema kuwa maneno ya Jaya ni ya kuudhi na yanapaswa kuangaliwa kwa umakini, kwani wao ni sehemu muhimu ya tasnia ya burudani na habari.

Hali hii imezidi kuleta mjadala mkali kuhusu heshima na haki za waandishi wa habari na waandishi wa picha, huku jamii ikihitimisha kuwa kila upande unapaswa kuheshimu nafasi na kazi za mwingine.

Related Articles

Back to top button